Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Farhad Abbasi, Naibu wa Utafiti wa Hawza za Kielimu, katika kikao chake na Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Sekretarieti ya Baraza la Wataalamu wa Uongozi (Majlisi Khobregan-e Rahbari) mjini Qum, alisisitiza kuimarishwa na kuingizwa rasmi kwa uhakiki ndani ya muundo wa kielimu wa hawza, na akatoa taarifa kuhusiana na kubuniwa programu za kina za kukuza ujuzi wa utafiti pamoja na malezi ya walimu watafiti.
Akiashiria mabadiliko ya msingi katika nyanja ya utafiti ndani ya hawza za kielimu, alisema: kwa bahati nzuri, utafiti ndani ya hawza za kielimu katika miaka ya hivi karibuni umepata uhai mpya. Leo, utafiti si tena jambo la awali au la pembeni, bali unaanzia ngazi za mwanzo na za kati, unaendelea hadi ngazi za juu kabisa za masomo ya hawza, na hata baada ya kuhitimu masomo, unaendelea katika mifumo mbalimbali iliyo na malengo mahsusi.
Naibu wa Utafiti wa Hawza za Kielimu aliongeza kuwa: kwa sasa, utafiti upo kama mkondo endelevu na wenye athari katika hatua zote za masomo ya kidini, na matukio muhimu yanajiri katika maeneo ya elimu ya utafiti, malezi ya watafiti, na uzalishaji wa elimu za kidini ndani ya hawza za kielimu. Mwelekeo huu ni mafanikio yenye thamani kubwa na ni chanzo cha fahari kwa hawza za kielimu.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Abbasi aliendelea kubainisha kuwa: leo, hawza za kielimu zimegeuka kuwa miongoni mwa vituo muhimu vya uzalishaji wa maarifa nchini. Ukuaji wa majarida ya kisayansi, vituo vya utafiti, maktaba na jumuiya za kielimu katika taasisi hii ya elimu ya dini umekuwa mkubwa sana.
Akiashiria hali ya hawza kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu, alisema: kabla ya mapinduzi, hawza zilikuwa na jarida moja au mawili tu kwa kiwango kidogo, lakini leo kwa fahari tunaweza kutangaza kuwa takribani majarida 280 ya kielimu yanachapishwa kwenye hawza za kielimu. Takriban majarida 70 kati ya hayo yamefanikiwa kupata viwango vya kielimu–utafiti na uenezi, na yanatekeleza jukumu muhimu katika uzalishaji wa maarifa ya kidini na elimu zinazohusiana nayo.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Abbasi, akitoa makadirio ya takwimu, aliongeza kuwa: hata kama kwa kiwango cha chini tutazingatia majarida 200 ya kisayansi yaliyo hai, na kila jarida likachapisha matoleo mawili kwa mwaka, tukizingatia wastani wa makala 6 katika kila toleo, basi kila mwaka takribani makala 2,500 za kielimu zenye ithibati hutayarishwa ndani ya hawza za kielimu. Baadhi ya majarida haya huchapishwa kwa mtindo wa kila robo mwaka, na hata kwa kuchapisha makala 8 katika kila toleo, jambo linaloonesha uwezo mkubwa wa kielimu na utafiti wa hawza.
Maoni yako